Uncategorized

Twaha Khassimu almaarufu “Twaha kiduku” ameibuka kidedea kwenye pambano la masumbwi la usiku wa deni lilifanyika jijini Dar es salaam.

Pambano hilo la raundi kumi lilimkutanisha na rafiki yake Abdalah Pazi almarufu “Dulla mbabe” ambaye licha ya kumpeleka chini Kiduku kwenye mzunguko wa kwanza alishindwa kufurukuta na kujikuta akipokea makonde mazito mfululizo licha ya kumudu kumaliza mizunguko yote kumi.

Hii ni mara ya pili mfululizo Kiduku anaibuka mshindi mbele ya Dulla mbabe.

Kuduku ambaye kabla ya kuwa bondia alikuwa muigizaji na mcheza ngoma za asili nyumbani kwao mkoani Morogoro.

Akiwa ameshinda mapambano 18 kati ya 20 aliyocheza Twaha Kassimu almaarufu Kiduku kabla ya kuingia kwenye masumbwi alikuwa mpiga ngoma za asili.

Ikiwa ni miaka minane toka alipopanda ulingoni kwa mara ya kwanza na kupata ujira wa shilingi elfu ishirini sawa na wastani wa dola tisa za Kimarekani anasema yeye anacheza ngumi kutafuta maisha licha ya kwamba awali familia yake haikuunga mkono.

Eagan Salla alimtembelea nyumbani kwao Morogoro Mashariki mwa Tanzania.

NO COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

Most Popular Article

To Top