Uncategorized

Kipchoge, ni mtu wa tatu kushinda mbio za masafa marefu matawalio katika michezo ya Olimpiki na kukamilisha mbio hizo katika muda wa saa mbili dakika nane na sekunde 38.

Mwanaridha huyo mwenye umri wa miaka 36 anayetambuliwa kama mkimbiaji bora zaidi, alivuka mstari dakika moja na sekunde 20 mbele ya Abdi Nageeye wa Uholanzi.

Katika mbio za kuwania taji la shaba mwanariadha wa Ubelgiji Bashir Abdi alimpiku Mkenya Lawrence Cherono.
“Nafikiria nimetimiza ndoto yangu kwa kushinda mbio za marathon kwa mara ya pili mtawalio. Natumai sasa kusaidia kuhamasisha kizazi kijacho, “mmiliki wa rekodi ya dunia Kipchoge alisema.

“Tokyo 2020 imefanyika, inamaanisha mengi. Inamaanisha kuna matumaini. Inamaanisha tuko kwenye njia sahihi ya maisha ya kawaida,” aliiambia BBC Michezo. “Tunaendelea na maisha yetu ya kawaida, ndiyo maana ya Olimpiki.
“Nina furaha kutetea taji langu na kuonyesha kizazi kijacho, ikiwa utaheshimu mchezo huo na kuwa na nidhamu unaweza kutimiza ndoto zako.”

Hii ni medali ya nne ya Olimpiki kwa Kipchoge,ambaye alipata umaarufu wa kukimbia mbio hizo kwa moda bora zaidi wa chini ya masaa mawili mwaka 2019.

Kipchoge alishindwa katika mbio hizo mara ya kwanza ndani ya miaka saba huko London mwezi Oktoba, lakini alichukua udhibiti wa mbio hizo mjini Sapporo, Japan, kabla ya kuingia kuonesha umahiri wake katika mbio hizo baada ya kukimbia kilomita 30.

Mkenya huyo – ambaye rekodi yake ya marathoni ni 2:01:39 alikimbia huko Berlin mnamo 2018 – alishinda shaba ya mita 5,000 mwaka 2004 na fedha mnamo 2008, kabla ya kushinda dhahabu yake ya kwanza ya Olimpiki huko Rio miaka mitano iliyopita.

Siku ya Ijumaa, Peres Jepchirchir wa Kenya alishinda mbio za marathon upande wa wanawake.

NO COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

Most Popular Article

To Top