Au kutakuwa na bingwa mpya kabisa?
Msimu mpya unapoanza mwishoni mwa wiki hii, mashabiki wameruhusiwa kuingia viwanjani, BBC inaangalia kwa namna gani timu tatu za juu zimejipanga na nini kingine kipya cha kutupia macho.
Barcelona inakombe moja la Copa del Rey – katika misimu yake miwili iliyopita ikiwa na Lionel Messi, lakini sasa inajiandaa kwa msimu mpya ikiwa bila ya gwiji lake hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Matatizo ya kifedha ya Barcelona, yaliyopelekea kushindwa kumbakisha mfungaji wake bora wa muda wote, licha ya kukubali kupunguza mshahara wake kwa 50% , aliteka vichwa vya habari vyote wiki iliyopita, kabla ya kuhamia Paris St-Germain.
Lakini kuna mengi ya kurekebisha yanakuja, huku mustakabali wa wachezaji wapya ukiwa haufahamiki bado.
Kuna wasiwasi kama wataweza kuwatumia wachezaji wake wapya wanne iliyowasajili ; Memphis Depay, Sergio Aguero, Eric Garcia au Emerson Royal.
Barcelona inapaswa kuwasilisha kikosi chake cha mwisho kitakachoshiriki laliga mpaka kufikia Septemba 1 – lakini wanapaswa kuuza kwanza wachezaji iliku kuwezesha wachezaji wapya kusajiliwa chini ya sheria ya Laliga ya kudhibiti viwango vya mishahara.
Kuumia kwa Aguero – kutakamfanya akae nje ya dimba mpaka Oktoba , ina maana huenda akawekwa kando kwa sasa.
Ikiwa kuna mambo mengi hayajakaa sawa, swali hapa namna gani mashabiki watapokea wakati huu wakiruhusiwa kuingia katika Nou Camp?
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mashabiki kuingia uwanjani tangu Koeman atue Barcelona – huku timu ikiwa katika wakati mbaya katika miaka mingi.
Kwa mantiki hiyo, Barcelona ikiwa bila mashabiki wake msimu uliopita wakionekana wazuri ugenini walikozoa pointi 41 kwenye La Liga msimu wa2020-21, wakati wakiwa nyumbani Nou Camp, walipata pointi 38.
Kocha mpya, ‘Uwanja’ mpya, na safu mpya ya Ulinzi Real
Real Madrid itarejea msimu huu ikiwa na safu mpya ya ulinzi baada ya kuwapoteza mabeki wake wa kati mapacha waliodumu kwa karibu muongo mmoja uliopita.
Sergio Ramos na Raphael Varane wamecheza pamoja Real Madrid katika michezo 227 ikiwemo mitatu ya fainali ya ligi ya mabingwa ULaya, wakishinda michezao 147, sare 43 na kupoteza 37.
Ramos amejiunga Paris St-Germain msimu huu alipomaliza mkataba wake na Real Madridi, huku Varane akitua Manchester United kwa ada ya £34m.
David Alaba anatarajiwa kuziba nafasi mojawapo, licha ya kuwa amecheza nafasi ya mlinzi wa kati katika robo tu ya michezo yote aliyocheza katika maisha yake ya soka. Nyota wa kimataifa wa Austria ndiye usajili pekee uliofanywa na Real Madrid majira haya, akitokea Bayern Munich tena bure.
Mbali na hilo,wamemrejesha kocha wao, Carlo Ancelotti kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane. Ancelotti aliiongoza klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa ulaya katika msimu wa 2013-14 , Ramos na Varane wakiongoza safu ya ulinzi na kutwaa pia ubingwa Copa del Rey.
Ni miaka minne sasa, tangu kocha huyo ashinde kombe, akipitia vilabu vya Napoli na Everton.
Mbali na hilo , wanatarajia kurejea uwanja wao wa nyumbani wa Bernabeu – unaoendelea kurekebishwa, katika mzunguko wan ne wa ligi, baada ya kupangiwa kuanzia ugenini katika michezo mitatu ya awali.
Kingine ni kwamba Gareth Bale amerejea klabuni, baada ya kuhitimisha mkopo wake pale Tottenham. Je msimu wake utakuwaje, ikiwa akiingia katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake?
Je Atletico Madrid itaweza kutetea ubingwa wake?
Caption: Diego Simeone kocha pekee kuingoza timu tofauti na Barca na Madrid kutwaa taji la La Liga tangu Rafael Benitez afanye hivyo msimu wa 2003-2003 akiwa na Valencia – amefanya hivyo mara mbili.
Hakuna timu zaidi ya Barcelona au Real Madrid iliyoweza kutetea ubingwa wa ligi ya La Liga tangu Athletic Bilbao ifanye hivyo mwaka 1984.
Atletico Madrid ina nafasi ya kufanya hivyo sasa baada ya kuipiku Real Madrid kwa alama mbili katika mbio za ubingwa msimu uliopita.
Wanarejea msimu huu wakiwa karibu na kikosi kile kile cha msimu uliopita – viungo Rodrigo de Paul na Marcos Paulo wakirejea pamoja na baadhi ya wachezaji waliokuwa nje kwa mkopo, akiwemo Vitolo leaving.
Kucheza soka kwa kiwancho cha juu kwa muda mrefu, linaweza kuwa jambo muhimu. Diego Simeo
ne amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kusalia kukinoa kikosi hicho, akikiongoza kutwaa mataji mawili kati ya manane yaliyopita
Atletico Madrid imekuwa kama na bahati ikimaliza juu ya msimamo wa ligi kwa ujumla na kufanya vizuri nyumbani kwa kupata alama 48 katika michezo 19 ukilinganisha na alama 38 ilizopata ugenini.
Je kuna klabu ingine inaweza kutwaa La Liga?
evilla inaweza kufanya vizuri kati ya zile zinazotajwa kuwania taji la ligi kuu ya Hispania msimu huu, ikimaliza nafasi ya nne msimu uliopita chini ya kocha, Julen Lopetegui.
Erik Lamela amesajiliwa akitokea Tottenham kuongeza nguvu ya kikosi hicho – lakini yeye na mlinda mlango Marko Dmitrovic, ndio wachezaji pekee waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa.
Je kusajiliwa kwa wachezaji hao itasaidia kupunguza pengo la alama 9 kati yake na Atletico? Wabashiri wengi wanaipa klabu hiyo nafasi ya nne.
Hakuna timu zingine zinazopigiwa chapuo kutwaa ubingwa. Ni timu nne tu za Real, Valencia, Getafe na Granada – zilizobadili makocha huku zikiwa hazijafanya usajili wowote wa kutisha msimu huu.
Mabingwa wa kombe la Europa Villarreal walimaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita, lakini usajili wake mkubwa msimu huu, Juan Foyth, alikuwepo kwenye kikosi hicho kwa mkopo
